Katika hali ya kusikitisha na kushangaza, watoto wawili wa kike wenye umri kati ya miaka saba na nane leo wameripotiwa kujilipua kwa mabomu waliyofungishiwa katikati ya soko kubwa Kaskazini – Mashariki mwa Nigeria.

Jeshi la Polisi la eneo la Mji wa Maiduguri jimbo la Borno, limesema kuwa shambulio hilo la bomu limetokea wakati watu wakiwa wamejaa kwenye soko hilo kufanya manunuzi na kwamba mtu mmoja amefariki na wengine 18 wamejeruhiwa.

Shuhuda wa tukio hilo ameiambia BBC kuwa wasichana hao waliofyatua vilipuzi walivyofungiwa nao waliuawa.

Ingawa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi hadi sasa, Kundi la Boko Haram ndilo linalonyooshewa kidole zaidi kwani limekuwa likitekeleza matukio ya mashambulizi ya mabomu ya kujitoa mhanga kwa kutumia watoto.

Jeshi la Nigeria liemefanya kazi kubwa ya kulidhibiti kundi hilo lakini bado limekuwa likifurukuta na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

 

Mourinho hataki mchezo, atangaza mazoezi mazito siku ya Christmas
Lowassa atumia Sikukuu ya Maulid kutoa ya moyoni kwa Wananchi, Watawala