Bosi wako wa zamani hafai kubaki katika historia yako tu. Katika kipindi hiki ambacho kupata fursa mpya inategemea uhusiano na mapendekezo kutoka kwa watu wenye sifa nzuri, kuwa katika mawasiliano na bosi wako wa zamani ni muhimu.

Anajuana na watu wengi, anajua historia yako ya kazi na anaweza kuthibitisha ujuzi na uwezo wa kazi zako wakati unahitaji utambulisho sehemu fulani.  Unaweza kuonekana una ubinafsi ikiwa utakaa kimya muda mrefu sana kisha kuja kumtafuta kuomba msaada. Ni sawa na kumtafuta mtu wakati wa shida tu.

Ingawa ni muhimu kuendelea kuwasiliana, unahitaji kuwa mwaangalifu katika hatua zako za kuwasiliana na mwajiri wako wa zamani ili kuepuka kutoelewana. BrighterMonday Tanzania wanakujuza njia rahisi za namna ya kuendelea kuwasiliana nae:

1. Mtakie Heri Wakati wa Likizo au Siku Muhimu

Kadi ni njia muhimu ya kuonyesha kuwa unamjali na kumkumbuka mtu. Andaa kadi maalum kwa Bosi wako wa zamani kumkumbuka siku muhimu kama vile kumtakia ‘Heri ya Siku ya Kuzaliwa’ au ‘Heri ya Mwaka Mpya’ japo mara moja kwa mwaka.

Zingatia kutuma kadi isiyoegemea upande wowote kidini kama hujui vyema kuhusu dini yake na hakikisha ujumbe wako uko wazi vizuri ili kuepuka kutokuelewana.

2. Wasiliana nae katika Mitandao ya Kijamii

Mitandao ya kijamii ni njia rahisi sana ya kuwasiliana na bosi wako wa zamani. Chagua mtandao sahihi unaofaa kuwaunganisha na tumia mahusiano ya kawaida na ya kitaaluma tu kuwasiliana nae.

Firikia juu ya aina ya uhusiano uliokua nao kabla ya kuondoka mahali pako pa kazi ili usije kuvuka mipaka. Hii itakusaidia kujua mtandao sahihi wa kuungana nae. Ikiwa baadhi ya mitandao kama vile Facebook na Instagram inaonekana kuwa ni ya kibinafsi zaidi, fikiria kuungana nae kwenye mitandao ya kitaaluma zaidi kama LinkedIn.

3. Mpe Taarifa Kuhusu Matukio Muhimu ya Maisha Yako

Si wazo baya kumshukuru bosi wako wa zamani kwa lolote lililopelekea wewe kufika hapo ulipo. Mpigie simu baadhi ya nyakati kumjulishe kwamba umepandishwa cheo, unahamia mkoa / nchi nyingine kikazi, au unabadilisha jina na anwani yako.

Unaweza pia ukamwalika kwenye matukio yako muhimu ya maisha kama vile harusi au utoaji shukrani kila mwaka. Hii ni njia nzuri ya kuwashukuru na inaweza kuwa kiungo muhimu kati ya fursa zako kitaaluma za siku za baadae.

4. Mjali kwa Makala Muhimu Zitakazomsadia

Unaweza kumfanya bosi wako wa zamani akuone unamjali na kumkumbuka kwa kumtumia makala na machapisho muhimu utakayokutana nayo mtandaoni. Mtumie barua pepe yenye kiungo (link) yenye makala nzuri, huku ukimwandikia ujumbe mfupi kama vile ‘Habari Bosi, nadhani utavutiwa sana na makala hii.’

Kumbuka kufanya barua pepe yako iwe fupi hakikisha kuna uwiano sahihi kati ya makala yako na umuhimu wako wa kutaka kuwasiliana nae.

5. Mwalike Mlo wa Mchana au Tembelea Ofisi yako ya Zamani

Ikiwa kazi yako mpya ulipata katika mji huo huo, unaweza kumualika bosi wako wa zamani kwa chakula cha mchana au kikombe cha kahawa katika mgahawa mara moja moja kwa mwaka. Ni njia nzuri sana ya kuongea mengi na kupata ushauri muhimu wa kazi zako. Ikiwa kazi yako mpya iko katika mkoa tofauti, siku ukipata nafasi ya kutembelea mkoa ulipo ofisi yako ya zamani, basi tafuta nafasi kupita kusalimia.

Ni nafasi nzuri pia ya kukutana na wafanyakazi wenzako wa zamani, na kubadilishana mengi.

Man Utd waweka mkono Sanchez kuachwa timu ya taifa
JPM ahoji ubaya wake upo wapi, awakumbusha haya wafanyakazi