Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Kenya (AIK) kimetishia kulishtaki Kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (PEFA), Nairobi kwa kile kilichotajwa kama uchafuzi wa kelele.

Rais wa Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Kenya, Harrison Mumia, amesema kimekuwa kikipokea malalamishi kuwa Kanisa la PEFA mtaani Saika hupiga kelele nyingi wakati wa kesha Ijumaa na siku ya Jumapili.

Katika barua iliyoandikwa Jumamosi, Januari 15, rais wa chama hicho, Harrison Mumia alilipa kanisa siku 14 kupunguza kelele ama lichukuliwe hatua za kisheria.

“Kelele kutoka kwa kanisa la PEFA haiwezi kuvumilika kwa wakazi wengi wanaoishi karibu nalo,” ilisoma barua iliyotumwa kwa Askofu John Okinda na Mchungaji Alex Wanyonyi.

Mumia aliongeza kuwa malalamishi hayo si ya wanachama wa AIK bali Wananchi Wakenya ambao wanahisi kanisa hilo linawaharibia starehe zao.

Awali, chama hicho kiliandikia Mamlaka ya Kuhifadhi Mazingira (NEMA), barua kikiitaka ifunge majengo ya ibada yenye kelele.

Mumia alisema maabudu hayo yanakiuka sheria zilizowekwa za kuzuia uchafuzi wa kelele.

Kulingana na taarifa iliyotolea siku ya Jumanne, Januari 19, 2021, wasiomwamini Mungu walisema walipokea malalamishi kutoka kwa Wakenya wakidai makanisa hayo yaliwakosesha amani.

Kwa mfano, Mumia alisema kuna misikiti ambayo huendesha ibada zao kila baada ya saa tano huku wakiwekwa vipaza sauti nje ya majengo yao.

Kwingineko, katika njia ya kuwavutia wanachama zaidi wasiomwamini Mungu, Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Kenya (AIK) kinawasijili wanachama wapya.

Katika notisi iliyotolewa na AIK, usajili unaendelea kwenye tovuti ya chama hicho kila mmoja akitakiwa kulipa ada ya KSh 500. Kujisajili, unatakiwa kuwa Mkenya mwenye zaidi ya umri wa miaka 18 ambaye hamuamini Mungu, uwe na utu na mawazo huru na Chama hicho kitagharamia bima ya afya ya wanachama wake na familia zao kwa kulipa KSh 20,000 na zingine KSh 20,000 za mazishi.

Mbinu nyingine wanayotumia kupata waumini ni ya mazishi ikiwa kimetangaza kuwa kitagharamia matibabu na mazishi.

Jamii hiyo ya wasioamini nchini Kenya (Atheists In Kenya) kimechukua hatua hiyo baada ya kupata pigo mwaka 2021 kufuatia katibu mkuu wake kujiuzulu na kuwa Mkristo.


Jamii hiyo imemsihi yeyote asiyeamini, anayeamini kwamba hakuna chochote kinachoweza kujulikana kuhusu uwepo au asili ya Mungu, mwenye mitazamo huru au anayetilia shaka mambo yanayoaminiwa, kujiandikisha kama mwanachama kupitia tovuti yao na kulipa ada ili kuweza kupatiwa huduma za kugharamia matibabu na mazishi.


Zaidi ya asilimia 97 ya raia wa Kenya ni wenye imani katika dini, kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya Pew.

Wanne washikiliwa kwa kula nyama za watu
Makalio makubwa kivutio cha wanaume