Serikali ya Wilaya ya Mtwara Mjini imewataka wafanyabiashara wilayani humo kutambua wajibu wao na kwamba hatua kali zitakuchuliwa kwa atakayekutwa hana Leseni wala kitambulisho cha msamaha wa Kodi kama ilivyoelekezwa na Rais Dkt. Magufuli

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda katika kikao na watendaji wa Kata na Mitaa wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kikao kilicholenga kuwahamasisha watendaji hao kutoa elimu kwa wananchi kuwataka kuchangamkia Vitambulisho vya wajasiliamali vilivyotolewa na Rais.

Amesema kuwa wajibu wa serikali ni kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabishara kuweza kuendesha shughuli zao kwa uhuru lakini pia wajibu wa wafanyabiashara hao ni kuhakikisha wanalipa kodi kwa walio na vigezo.

“Kila mtu anayefanya shughuli zake ajulikane hasa kama anafanya biashara/Mjasiriamali, kama ni mfanyabiashara mkubwa mtakua mnamfahamu, kama ni Mdogo mnamfahamu kwasababu jitihada za serikali ni kurasimusha wajasiliamali wadogo kwa kuwapa vitambulisho ili waweze kuingia kwenye mfumo wafahamike,Amesema DC Mmanda.

Aidha, amesema Msimamo wa serikali ni kutambua shughuli zote zinazofanyika ukizingatia tayari ilishatolewa miongozo na viongozi wa kitaifa juu ya wajibu wa Wafanyabiashara ikiwemo kuwatambua wajasiliamali wadogo ambao wamepewa vitambulisho vya msamaha wa Kodi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni amewataka watendaji hao wa Kata na Mitaa kuendelea kuwajibika katika nafasi zao hususani kuhamasisha wananchi wanao waongoza juu ya zoezi hilo la Vitambulisho.

Hata hivyo, Serikali wilayani Mtwara imetoa msisitizo kwa Wajasiliamali hao kuitikia wito kwa kuchukua vitambulisho hivyo vilivyotolewa  na Rais ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokjeza.

Wapinzani kung’ang’ana na sakata la Sh. 1.5 trilioni majimboni
CCM Njombe yaadhimisha miaka 42 kwa kupanda miti