Mtoto wa miaka 10 mwananfunzi wa darasa la nne shule ya msingi Katisungu aliyejulikana kwa jina la Levana Oscar amefariki dunia baada ya kubakwa na kupigwa jiwe kichwani na mwili wake kutupwa porini na watu wasiojulikana.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Society Halmashauri ya Nsimbo mkoani katavi baada ya mtoto huyo kwenda kuchota maji kwenye dimbwi lililopo pembezoni mwa makazi ya watu.

Mganga mfawidhi wa wa zahanati ya Magamba Shamu Adamu Isike, alisema baada ya kufika eneo la tukio na kufanya vipimo ilionekana ni kweli mtoto huyo kafanyiwa vitendo hivyo vya kiukatili.

Mfuga nyoka afariki dunia baada ya kung’atwa na nyoka

Hata hivyo amesema kuwa inawezekana mtoto huyo aliwafahamu wahusika wa tukio hilo baada ya kumbaka.

”Kabla ya uchunguzi wa ndani mtoto alionekana amepigwa jiwe kwa nyuma maeneo ya kichwani hadi kupoteza maisha ila baada ya kufanya vipomo niligundua kweli alibakwa” amesema Dk Isike.

Baba wa mtoto huyo Oscar Charlse Nyansio amesema kutokana na maumivu aliyonayo kuhusu kifo cha mwanae anaiomba serikali imsaidie kupatikana kwa kwa wahusika wa tukio hilo.

Mkuu wa majeshi Niger afukuzwa kazi

Hata hivyo tukio hili linafananishwa na tukio jingine ambalo lilitokea mwaka jana katika eneo la Makanyagio mkoani hpo ambapo mwanamke  mmoja alibakwa hadi kufa wakati akitokea dukani kununua mafuta ya taa majira ya usiku.

Mashtaka ya Donald Trump kuwasilishwa rasmi mbele ya Bunge la Seneti
Mfuga nyoka afariki dunia baada ya kung'atwa na nyoka

Comments

comments