Mahakama ya Mwanzo Uyole jijini Mbeya imeungua kwa moto na kuteketeza kila kitu mahakamani humo ikiwemo taarifa na mafaili yote ya kesi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka mahakamani hapo tukio hilo limetokea usiku wa Mei 5 ambapo hadi kufikia majira ya saa tatu kila kitu katika mahakama hiyo kilikuwa kimeteketea.

Hata hivyo Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na wakazi wa Uyole ya kati ilipo mahakama hiyo wameshirikiana kuzima moto huo lakin jitihada hizo hazikufanikiwa.

Chanzo cha tukio hilo hakijafahamika mara moja lakini hakuna madhara yoyote ya kibinadamu yaliyotokea na viongozi mbalimbali wa serikali ya mtaa na kata wamefika eneo hilo na kuwashukuru wananchi walivyoshirikiana na jeshi la zimamoto kuzima moto huo licha ya kwamba mahakama na kumbukumbu zote kuteketea kwa moto huo.

TAMISEMI yawaonya wanaombeza Makonda
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 6, 2018