Sheria ndogo imepitishwa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga itakayomlazimu binti anayetaka kuolewa kuonyesha cheti cha kuzaliwa kwanza kitakachomwezesha mwenyekiti kutoa kibali ama la.

Uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kuona tatizo la mimba na ndoa za utotoni linaendelea kushamiri kwenye wilaya hiyo, hivyo wakaona ni vyema kutunga sheria ndogo itakayo wabana wazazi kushindwa kuozesha watoto wao wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Sheria ya ndoa ya mwaka (1971) sio rafiki kabisa kumlinda mtoto wa kike, inaruhusu kuolewa akiwa chini ya umri wa miaka 18 kwa ridhaa ya wazazi wake au mahakama, hivyo kulazimu kuwepo kwa ndoa nyingi za utotoni ambazo hukatisha ndoto za watoto wa kike,”amesema Ngassa Mboje mwenyekiti wa halmashauri hiyo

Aidha, Ofisa Mradi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga, Mustapha Isabuda amesema kuwa wameamua kukutana na madiwani hao baada ya kuona tatizo hilo linazidi kuongezeka.

Hata hivyo, kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi amelipongeza shirika la Agape kwa kumpigania mtoto wa kike.

 

Video: Mikopo elimu ya juu wabunge wachachamaa, Makinikia yaleta kiama
Mwijage adai Propaganda zimekutana na 'Propagandist' aliyesomea China

Comments

comments