Mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika serikali ya awamu ya nne na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM, Stephen Wasira amesema kuwa hawawezi kufanya siasa bila ya kukitaja chama cha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa ndio shetani wao.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika Jijini Dar es Salaam baada ya kusikia kauli ya mgombea Ubunge wa Chadema kuwa CCM hawawezi kufanya siasa bila ya kuitaja CHADEMA.

“Nimemshangaa kiukweli mgombea huyo, maana hata Maimamu na Wachungaji huwa hawawezi kumaliza ibada bila ya kumtaja shetani maana shetani ndio mpinzani wao na endapo wasipotaja wana kuwa hawajamaliza ibada yao. Hivyo asishangae sana na sisi tunapokuwa katika siasa kuitaja CHADEMA kwa maana ndio shetani wetu hapa,”amesema Wasira

Hata hivyo, Wasira amesema tokea mwaka 2015 kumekuwa na siasa za kishetani nchini Tanzania hasa upande wa upinzani ambazo zimetawaliwa na uongo unaofanana na giza kwa kusema uongo katika kampeni zao na kudanganya wananchi.

 

Lowassa awaziba midomo Chadema
Magazeti ya Tanzania leo Januari 28, 2018

Comments

comments