Kada wa Chama cha Mapinduzi, Steven Wasira amesema kuwa wapinzani wamekosa hoja za kuongelea hivyo wamebaki kupiga kelele.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.

Amesema kuwa dhana ya kusema kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa hizo ni propaganda ambazo wamekuwa wakizieneza makusudi.

“Hawa jamani sasa hivi wanatapa tapa tu, wameishiwa hoja, ndio maana kila siku wanakimbilia kwenye mitandao kutukana viongozi wa nchi,”amesema Wasira

Kwa upande wake, Mustaph Muslim aliyehamia chama hicho akitokea chama cha demokrasia na maendeleo, amemshauri Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchema kumshughulikia Mange Kimambi anayeishi nchini Marekani.

Uchaguzi: Chadema msiondoe macho kwenye ‘mpira’ mtamlaumu refa
BFT: Si kweli timu ya taifa inaishi kwa chai na chapati