Wasomi wamechambua msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wa kusema kuwa kwa sasa anajenga nchi na kuutupilia mbali mchakato wa katiba mpya ambao ulikuwa umeanza kutoka awamu ya Nne na kuligharimu taifa  fedha nyingi ambapo wananchi walitoa maoni yao.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Hellen Bisimba amesema Rais Magufuli kusitisha mchakato wa katiba ni kulipatia hasara taifa, amesema inasikitisha  sana kwa Rais kusema hana mpango na mchakato wa katiba wakati umegharimu taifa fedha nyingi kuufikisha hapo ulipofikia na kuongeza kuwa hapa tulipofikia tunahitaji katiba mpya.

Aidha, kwa upande wake Prof. Safari amesema Rais Magufuli anarudisha nyuma maendeleo ya nchi na wala haisaidii Tanzania kusonga mbele na kuongeza kuwa pesa zilizotumika kuandaa mchakato wa katiba ni nyingi hivyo Rais anatakiwa aweke kipaumbele wa suala la mchakato wa katiba ya wananchi.

Hata hivyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Benson Bana amesema kuwa  ni vyema watanzania watambue kuwa katiba inahitaji utulivu na umakini wa hali ya juu ili kuweza kuunda katiba yenye manufaa  kwa nchi na watanzania kwa ujumla.

 

Pacquiao kuzichapa na Vargas saa chache zijazo, ni pambano lililobeba historia
Vuguvugu la Trump, Clinton kuingia 'White House' lapamba moto