Aliyekuwa waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika Serikali ya Awamu ya Nne, Stephen Wassira amemvaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Mkamba kufuatia kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa serikali iliyopita iliendeshwa kwa kuleana, kuoneana haya na kusitiriana.

Wassira amepinga vikali mtazamo huo wa Makamba akieleza kuwa hakukuwa na kubebana na kuoneana haya kama anavyoeleza kwani yeye alifanya kazi nzuri kutekeleza majukumu yake kikamilifu siku zote.

“Labda alilelewa yeye…kama rafiki yangu Makamba anasema kulikuwa na kuleana, mimi kwa upande wangu sikulelewa nilifanya kazi na nikatimiza wajibu wangu kama nilivyopewa na Rais,” Wassira aliwaeleza waandishi wa habari hivi karibuni nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo alienda mbali na kugusia suala la Makamba kuingia kwenye nafasi ya ‘Tano Bora’ kwenye mchujo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpata mgombea urais, akidai kuwa kuna taarifa kuwa alibebwa.

“Na yeye inawezekana alilelewa maana kuna watu wanasema kuingia kwake tano bora ya urais alipendelewa labda huko ndio kulelewa ndio maana akasema hivyo,” anakaririwa.

Wassira alikuwa miongoni mwa makada wa CCM waliochukua fomu ya kuwania nafasi ya kugombea urais kupitia chama chao na pia aliongoza jopo la uandishi wa Ilani ya chama hicho ya mwaka 2015.

 

Wauguzi 'wanusa moto' baada ya mzazi kujifungulia kwenye beseni akiwa hospitalini
Samia Suluhu asema mgogoro wa Zanzibar umesababishwa na 'wana CCM, mamluki'