Wastaafu 332 waliokuwa wafanya kazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wameiomba Serikali kuinglia kati  ili waweze kulipwa kiinua mgongo chao cha tangu mwaka 1978.

Wastaafu hao wamesema kuwa wamefikia hatua hiyo ya kuiomba Serikali kuingilia kati baada ya kuambiwa wasubiri majina yao  kwaajili ya uhakiki tangu februari hadi  Novemba mwaka huu.

“Mwanzoni mwa mwaka huu, tulipata taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuwa wastaafu waliofanya kazi Muhimbili tangu mwaka 1977, wafike kwaajili ya kuhakiki majina yao na kisha kuleta nakala za malipo ya awali, lakini cha kushangaza anatuambia hatuna madai, jambo ambalo mpaka sasa hatuelewi”amesema Mzee kumbakumba.

Kwa upande wake mstaafu mwingine, Modestus Mwampeta, amelalamika kwa kutolipwa  mafao yake licha ya kufanya kazi kwa miaka 42 na kwamba kwa sasa wananyimwa kiinua mgongo na kupata usumbufu mkubwa kutoka vijijini kuja mjini kufuatilia mafao.

“Tulivyofika Muhimbili kama wito ulivyotolewa, tuliambiwa tuandike taarifa zetu na walichukua muda mrefu zaidi ya miezi saba, leo wanatuambia hatudai chochote Muhimbili”amesema Modestus.

Hata hivyo kwa upnde wake Ofisa Mahusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligeisha, amesema kuwa wastaafu hao hawadai chochote na kwamba walishaushitaki uongozi wa Hospitali ya Muhimbili mahakamani na tayari hukumu ilishatolewa, ambapo wameshindwa.

“Hakuna chochote wanachodai, ikizingatiwa walikwenda wakaishitaki MNH na walishindwa katika kesi,hakuna wanachodai”amesema Aligeisha.

Ukata wamtupa jela miezi 6 Diwani wa CUF
JPM afyeka 230 NEC, 10 Kamati Kuu CCM