Muigizaji wa mrembo, Wastara Juma ameamua kuweka wazi kinachoendelea katika maisha yake baada ya mguu wake kukatwa miaka 6 iliyopita.

Watara ambaye hivi sasa yuko jijini Nairobi aliamua kupost kwenye Instagram picha pamoja na maelezo yanayokanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa alikatwa miguu yote miwili.

Wastara

Hivi ndivyo alivyoandika:

“Kwa mara ya kwanza toka nimekatwa mguu miaka 6 iliyopita leo nimechukua nafasi hii kupost hii pic [hapo juu] kuondoa maswali mengi yaliyopo vichwani mwa watu

Nipo kma unavyoiona pic

Huyo ndio wastara nilivyo hakuna kilichopungua zaidi ya hicho unachokiona

Kuwa mlemavu ni kitu kingine tofauti ukiwa mzima hivyo kusikia maumivu na kuumwa mguu ni kitu cha kawaida

Sasa nipo nairobi kimatibabu na tatizo ni operetion ya kwanza nilikosewa ndio sababu ya maumivu ya mara kwa mara madaktari wameshajua nini cha kunifanya ili kuondoa mateso kwangu

Jifunze kitu kupitia hii pic yangu na si kucoment ujinga jiulize ungekuwa wew mama yako dada yako mume, , wako ungeweza kusmile kma mimi hali ya kuwa una maumivu?

Jifunze kitu kupitia wastara  na sijajidharirisha nimetaka wew unijue nilivyo ili usiteseke na maswali juu yangu Sijakatwa miguu yote kma ilivyovumishwa na pia pamoja na maumivu ninaweza kutembea japo si mwendo mrefu sana na naendelea kusmile

SOTE TUSEME ALHMADULILAH

ASANTE MUNGU”

Picha: Mjamzito Akining’inia Dirishani Kuwatoroka Magaidi Ufaransa
Picha: Justin Bieber Amwaga Machozi Jukwaani Kuililia Ufaransa