Msanii wa filamu za bongo, Wastara Juma ambaye hivi karibuni amepewa mchango wa milioni 15 na familia ya Rais Magufuli, amewajibu watu waliokuwa wakimtuhumu kuwa tapeli na kwamba hana ugonjwa wowote unaomsumbua.

Amesema kuwa kabla ya kuomba michango alijitahidi sana kujitafutia mwenyewe hiyo pesa kwani hakutaka pesa ya mtu mwengine ije imsaidie, kwakuwa alijiona kama ni mzigo kwa jamii.

Aidha, Wastara amesema alishajaribu kujiingiza kwenye biashara ambazo amedai hazina faida, mpaka kufikia hatua ya kuanza kuuza vitu vya ndani, jambo ambalo msanii mwenzake Steve Nyerere alimkataza, na kumshauri aweke wazi matatizo yake iili watu wamsaidie.

Hata hivyo, amelalamikia kitendo cha watu kumdhihaki, huku akisema asilimia kubwa ya watu wanaomtuhumu hawajawahi hata kwenda kumuona wakiwemo wasanii wenzake, ambao waliamua kumtenga baada ya yeye kuolewa na aliyekuwa Mbunge wa CCM Sadifa.

 

Trump amjibu Jay Z kuhusu Afrika na ‘Wamarekani Weusi’
Apigwa risasi kichwani wakijaribu kushuti video waweke Facebook