Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza kinachofanya utafiti wa dawa ya corona, kimesema kuwa kimefika hatua nzuri ya kupata dawa hiyo, lakini wana changamoto ya kuwapata watu wa kuwafanyia majaribio hapo baadaye kwani virusi hivyo vimeanza kutoweka kwa kasi.

Profesa anayeongoza jopo la watafiti wanaotengeneza dawa hiyo ameliambia gazeti la Telegraph kuwa majaribio ya dawa iliyoandaliwa yatafanywa kwa watu 10,000 waliojitolea, lakini hadi sasa kuna 50% kuwa huenda wasiipate idadi hiyo siku za usoni kwakuwa watu wengi wanapona.

“Ni mbio kali za kufikia mafanikio wakati ambapo maambukizi yanapotea nchini kwa kasi. Hadi sasa kuna 50% ya kutopata matokeo kamili hapo baadaye,” Andrian Hill, Mkurugenzi wa Taasisi ya Jenner ya Oxford iliyoungana na AstraZeneca Plc ambao ni watengenezaji wa dawa amekaririwa na Telegraph.

Dawa hiyo inayofanyiwa majaribio, inayoitwa ChAdOx1 nCoV-19, ni moja kati ya dawa zilizo katika mstari wa mbele kwenye mbio ya dawa zinazoandaliwa kuwa kinga dhidi ya covid-19.

Timu hiyo imeanza kufanya majaribio ya awali ya dawa hiyo Aprili, 2020 na hadi sasa ndiyo dawa pekee iliyotangazwa inayoonekana kufika katika hatua ya juu zaidi.

Jumla ya visa vya corona vilivyothibitishwa hadi sasa ‘UK’ ni 259,559, na siku ya Jumapili maabara ilitoa majibu ya visa 2,409, kwa mujibu wa tovuti ya Serikali.

Sky News wameripoti kuwa kushuka kwa kasi kwa maambukizi mapya ya corona ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwanzoni, inawafanya watafiti kuhofia kuwa huenda wakapata wagonjwa wachache zaidi ya wanaohitajika kufanya majaribio ya kutosha ya dawa yao. Hivyo, huenda watafiti hao wakakosa ushahidi wa kutosha wa kisayansi kuthibitisha ufanisi wa dawa yao kwa uchache wa majaribio.

India yarejesha safari za ndege leo, changamoto nyingine yaibuka

Shule za msingi kufunguliwa Juni 1 – Uingereza

Makonda ataka mkandarasi kukabidhi stendi ya Mbezi kwa wakati
India yarejesha safari za ndege leo, changamoto nyingine yaibuka