Kikosi cha wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya nishati ya atomiki, kimeelekea kwenye kituo cha nishati ya nyuklia nchini Ukraine, baada ya miezi kadhaa ya mvutano ulioongezeka kati ya vikosi vya Ukraine na Urusi, vinavyoshtumiana kukishambulia kwa makombora kinu cha Zaporizhzya.

Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki (IAEA), Rafael Grossi amesema anajivunia kuongoza ujumbe wa msaada na usaidizi wa shirika hulo kwenda Zaporizhzya, kwenye mtambo ambao umekuwa ukidhibitiwa na vikosi vya Urusi tangu muda mfupi baada ya uvamizi wao nchini Ukraine.

Amesema, “Siku imefika ya kulinda ulinzi na usalama wa mtambo huo, ambao ni mkubwa zaidi barani Ulaya.” Huku akiandika maoni yake katika mtandao yaliyoambatana na picha yake na wafanyakazi wengine 13 wa IAEA, kabla ya kuanza safari yao.

Mara baada ya IAEA kuwasili Zaporizhzya, Grossi amevitaja vipaumbele vya wataalam hao kuwa ni pamoja na kufanya tathmini ya uharibifu na kuangalia kama mifumo ya ulinzi na usalama inaendelea kufanya kazi.

Taarifa zilizopokelewa kutoka Ukraine na Urusi, kuhusu hadhi ya kituo hicho zimekuwa zinakinzana ambapo IAEA ilibainisha wakati huo, kuhusu uendeshaji wake na uharibifu unaoendelea.

Taarifa kutoka kwa kituo cha uratibu wa pamoja (JCC), inayohusisha Ukraine, Urusi, Türkiye na Umoja wa Mataifa kiliripoti kuwa jumla ya safari 114 zimewezeshwa hadi sasa (62 za ndani na 52 za nje), tangu makubaliano hayo yatiwe saini tarehe 27 Julai mwaka huu mjini Istanbul, Uturuki.

Ukame tishio jipya la uchumi wa Ulaya
Serikali, PLF waitwa meza ya mazungumzo