Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi ametoa rai kwa wataalamu 79 waliohitimu mafunzo ya uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuhakikisha wanalitumikia Taifa kwa weledi na uzalendo mkubwa ili kutekeleza ajenda ya uchumi wa kidijiti.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti wataalamu hao jijini Dodoma, Dkt. Yonazi amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanafanya vizuri katika maeneo yao ya kitaaluma na kuishauri Serikali nini kifanyike ili Mkongo wa Taifa uendelee kuleta ushindani wa kiuchumi utakaoleta tija kwa Taifa na wananchi kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya uendeshaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wataalamu 79 kutoka Wizara ya Ulinzi na Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL) jijini Dodoma.

Amesema, “Ni heshima kubwa kupata fursa ya kuitumikia nchi, kuhitimu mafunzo haya sio kwa ajili ya kupata cheti tu, bali kuboresha mwenendo na utendaji wenu katika kutumikia taaluma na ujuzi mlioupata kwa manufaa ya nchi.”

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia ya TEHAMA wataalamu hao wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kujifunza mara kwa mara ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na kuwa chachu kwa wengine.

Umoja Kenya: Viongozi wa Dini wapewa jukumu
Saba wauawa kwa shambulio la risasi kwenye Ibada