Waziri wa afya, Ummy Mwalimu, amezindua kituo cha huduma za Simu kwa wateja “Afya call centre” ikiwa ni sehemu ya jitihada za wizara kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masuala mbalimbali ya Afya.

Akizindua huduma hiyo jana, waziri ummy amesema Kwa sasa kipaumbele ni taarifa na Ushauri kuhusu ugonjwa wa covid 19.

Amebainisha kuwa kituo hicho kitahudumia jamii kwa saa 24 na kitakuwa na wataalamu 50 kwa wakati mmoja wakiwemo Madaktari, Wauguzi na Wanasaikolojia.

Ummy ametoa rai kwa wananchi wakatakaopiga simu bure (namba 199) kujenga ustaarabu wa kutumia lugha ya staha pamoja na kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia Serikali na wizara ya afya kuchukua hatua stahiki na kwa wakati.

Aidha amebainisha kuwa kitatumika kutoa Taarifa kuhusu masuala mengine ya Afya ikiwemo huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Taarifa za magonjwa ya Malaria,TB, VVU/UKIMWI.

Miaka 75 ya kumalizika vita ya pili ya dunia, Corona yaingilia ratiba
Ujumbe wa mwisho wa marehemu OCCID Masoud "Allah atujalie mwisho mwema''