Wachunguzi kutoka Shirika la kudhibiti silaha za sumu OCPW walioenda nchini Syria wamenyimwa kibali cha kuingia katika mji wa Douma kuchunguza madai ya shambulizi la silaha za kemikali mjini humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Shirika hilo la OCPW, Ahmet Uzumcu katika mkutano wa hadhara, ambapo amesema kuwa wachunguzi hao wamekosa kibali cha kuingia katika mji yalikofanyika mashambulizi hayo mjini Douma.

Amesema kuwa Serikali ya Syria pamoja na Urusi wamewanyima nafasi wachunguzi hao kuingia mjini humo kwa sababu za kiusalama, ambapo amesema kuwa mpaka sasa bado hawajaweza kuhakikishiwa usalama wao na haijawekwa wazi ni lini hasa hilo litakapofanyika.

Hata hivyo Urusi na Syria zimekanusha madai ya kuwanyima kibali cha kuingia na kufanya uchunguzi katika mji huo wa Douma.

 

Video: Balaa la Mvua, Ripoti ya CAG yavuruga Bunge
Makamishna wa Tume ya Uchaguzi wajiuzulu

Comments

comments