Watafiti wa Mikoa ya Kaskazini nchini wamegundua programu maalum ya simu itayomuwezesha daktari ama muuguzi kutumia simu yake ya kisasa (smartphone) kusaidia kuchunguza saratani ya kizazi, ugunduzi unaotajwa kuwa wa kipekee na wa kwanza duniani.

Kwa mujibu wa watafiti hao, daktari ama muuguzi katika kituo chochote anapaswa kutumia simu yake ya kisasa baada ya kuunganisha (ku-install) programu hiyo maalum, kupiga picha eneo la mfuko wa uzazi na kisha kutuma picha hiyo kwa kutumia program hiyohiyo kwa mtaalam aliye kwenye kliniki husika.

Imeelezwa kuwa baada ya kupokea picha kupitia program hiyo, wataalam wataichunguza na kutoa majibu pamoja na maelekezo ya kitabibu kama ambavyo wangeweza kufanya baada ya kupima mgonjwa husika.

Ili kukwepa tatizo la uhafifu wa mtandao, muuguzi anaweza kupiga picha hiyo na kuitunza kwenye simu na kisha kuituma pale mtandao utakapokuwa wa uhakika.

Program hii inaonekana kuwa endapo itafanikiwa kwa kiwango kinachotarajiwa, itakuwa msaada mkubwa katika kupambana na ugonjwa wa saratani ya kizazi nchini ambapo zaidi ya wanawake 4000 wanadaiwa kupoteza maisha kila mwaka nchini kwa ugonjwa huo, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Chanzo: BBC

Msajili wa vyama vya siasa awageukia wadau wa habari na kutoa onyo kali
Kubenea apandishwa kizimbani kwa ‘habari za uongo’