Klabu ya Simba SC imeanza vibaya mchezo kati yake na watani wake wa Jadi kutoka Jangwani, Yanga SC unaoendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kubamizwa goli 1 -0 katika kipindi cha kwanza.

Goli hilo limefungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 39 ya mchezo huo. Mchezaji huyo raia huyo wa Zimbabwe amekamilisha lake la 11 katika msimu huu wa Ligi. Goli hilo linatajwa kama ‘goli rahisi kwenye mechi ngumu’.

Kosa la Mlinzi wa Simba, Ramadhani Kessy ndilo lililompa nafasi Ngoma kuudonoa mpira na kuupachika nyavuni bila kutumia nguvu kubwa.

Simba wanaonekana kuwa katika wakati mgumu zaidi baada ya mchezaji wake Abdi Banda kupigwa kadi nyekundu, hivyo kuwafanya wacheze wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja dhidi ya wana Jangwani.

Yanga wamecheza makosa 7 huku Simba wakifanya makosa 10 yaliyosababisha faulu huku mawili kati ya hayo yakiwagharimu kuondolewa kwa mchezaji wake, Abdi Banda.

Mpira dakika 90, lolote linaweza kutokea.

Matokeo Rasmi Uganda: Museveni atangazwa mshindi
Donald Trump awashawishi watu kuigomea Apple