Watu watano wa familia moja wakazi wa kijiji cha Zanka, Wilayani Bahi Mkoani Dodoma wamekutwa wameuawa na watu wasiojulikana

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma RPC.Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kufika katika eneo la tukio ambapo miili ya watu hao imekutwa ikiwa ndani ya nyumba yao walimokuwa wanaishi ikiwa tayari imeharibika.

Waliouwawa ni pamoja na Baba, mama, watoto wawili na mjukuu mmoja.

Akizungumza Mara baada ya kufika eneo la Tukio Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka amelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza mara moja Uchunguzi kubaini watu waliohusika kufanya mauaji ya watu hao watano wa familia moja

Haya ndo madhara ya ngono ya mdomo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 23, 2022