Leo July 23, 2018 Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa watano baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa makusudi mfanyabiashara wa Arusha na Mirerani, Erasto Msuya.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni mshtakiwa Sharifu Mohamed, Mussa Mangu, Karim Kuhundwa, Sadick Mohamed na Ally Mussa Majeshi.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi hiyo.

Pia, Mahakama imemwachia huru mshtakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.

AC Milan kuitibulia Chelsea kwa Gonzalo Higuain
Jose Mourinho amfungia milango Anthony Martial