Vijana 11 raia wa Tanzania waishio Johannesburg nchini Afrika Kusini walioshtakiwa kwa kosa la ubakaji wameachiwa huru na hakimu mkazi wa Mahakama ya Johannesburg.

Watanzania hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kumteka nyara na kumbaka mwanamke mjamzito Thelma Mondowa raia wa Zimbabwe mwaka jana.

Aidha, Wakili wa upande wa mashtaka wa serikali amemfahamisha hakimu kuwa Bi Thelma Mondowa aliamua kuondoka Afrika Kusini na kurejea Zimbabwe na wameshindwa kupata ushahidi wa kutosha.

Inasemekana kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka kazini na mfanyakazi mwenzake wa kiume ndipo ghafla walipovamiwa na kundi la watu wenye silaha na kumvuta mwanamke huyo kabla ya kumpiga mfanyakazi mwenzake ambae baadaye alifanikiwa kutoroka.

Hata hivyo, baada ya mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu polisi na wakafanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wanaume hao wakimbaka kwa zamu mwanamke huyo.

Diogo Dalot anukia Old Trafford
Magazeti ya Tanzania leo Mei 30, 2018