Baada ya sampuli 1,116 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita, Uganda imetangaza wagonjwa wapya 31 wa covid -19 waliopatikana na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253.

Wizara ya Afya nchini humo imesema kati ya wagonjwa 23 waliopatikana mipakani, 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na 4 ni Wakenya. Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao.

Wagonjwa 23 wa kutoka mipakani wamepatikana baada ya sampuli 896 kuchukuliwa na 8 ni walipimwa wakiwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali kuwa na virusi vya corona.

Aidha, Wizara imebainisha kuwa hadi kufikia sasa jumla ya Wagonjwa 69 wamepona na hamna kifo.

Young Africans kuanza mazoezi leo
Ndayishimiye ahutubia taifa kwa mara ya kwanza kama Rais