Katibu mkuu wa wizara ya Afya (Utawala), nchini Kenya, dkt. Rashid Aman amethibitisha visa vipya vya Corona kwa madereva wa maroli 25 katika mpaka wa Namanga wakiwepo watanzania.

Amesema kati ya madereva hao, 23 ni watanzania, mmoja ni raia wa Rwanda na mmoja ni Mganda na wamekataliwa kuingia nchini Kenya baada ya vipimo vilivyofanywa mpakani Namanga kuonesha wana maambukizi ya covid 19.

Amesema wamezuiwa kuingia nchini humo ili kulinda wakenya, Katibu huyo amefafanua kuwa kila nchi mwanachama wa jumuiya ya EAC inajukumu la kulinda watu wake, hivyo Kenya itaendelea kuwalinda Wakenya.

Mbowe na wenzake kusuka au kunyoa kesho, Spika awapa masharti
Sarpong kufanya maamuzi