Watu watatu wamefariki dunia, katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Loitoktok nchini Kenya, baada ya pikipiki waliyokuwa wakisariria kugongana na pikipiki nyingine.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Loitoktok, Shadrack Ruto amesema ajali hiyo ilitokea siku ya Ijumaa Septemba 16, 2022 majira ya saa mbili usiku.

Ajali ya Pikipiki.

Amesema, katika tukio hilo watu wawili waliaga dunia eneo la ajali, na abiria aliyekuwa amebebwa kwenye pikipiki nyingine alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali, mjini Loitoktok.

“Waendeshaji wanashukiwa kuwa kwenye mwendo wa kasi sana walipogongana, na wahusika wote wanakisiwa kuwa raia wa Tanzania kutokana na nambari za usajili za pikipiki hizo kuonesha zimesajiliwa nchini humo,” ” Amesema Kamanda Ruto.

Ruto akataa wapinzani kwenye serikali yake
Jina la Lukuvi lamkamatisha tapeli