Watanzania wameshauriwa kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara zinazojitokeza katika soko la China, ili kuweza kujiongezea kipato na kuinua uchumi wa mtu mmoja mkoja na Taifa zima kiujumla ikiwemo bidhaa za uvuvi ambazo zinapendwa na watu wengi kutokana na ubora wa malighafi husika.

Uchangamkiaji wa fursa hizo unatokana na mkataba ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alishududiwa ukisainiwa wakati wa ziara yake nchini China Novemba 3, 2022 , ambao unafufungua fursa mpya za uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo samaki aina ya Sangara wanaotumika zaidi kwa ajili ya kitoweo katika Taifa hilo.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki kupitia taarifa yake kwa umma juu ya bidhaa za uvuvi kutoka Tanzania zinazohitajika kwa wingi katika soko la China ikiwemo pia bidhaa nyingine za uvuvi zinazofanyika nchini hapa ambapo hadi kufikia sasa Makampuni 72 yameshasajililiwa ili kuuza kazi hiyo.

Familia ikipata kumbukumbu ya picha jijini Beijing China. Picha ya

Amesema, “Zikiongezeka Kampuni nyingine zaidi ya hizo 72 itakua imesaidia kujikwamua kiuchumi kwa vijana wetu na hata Taila letu na kuzalisha ajira kwa Watanzania wengi. kwa faida ya watanzania kuchangamkia fursa zipo bidhaa 12 ambazo zinahitajika kwa wingi hapa China ikiwemo ya Samaki Salmon, Bokuruti na Ribon Fish.”

Hata hivyo, Balozi Kairuki ametoa angalizo kwa Watanzania wanaotaka kuuza bidhaa zao nchini China kuhakikisha wanafanya usajili wa Kampuni kwani bila kufanya hivyo bidhaa zao zitateketezwa, na kwa wale wasio na Kampuni kushauriwa kuziuza kwa wale waliosajili kihalali ili ziweze kuwapatia faida na kwamba watatoa bei elekezi ili ziwasaidie kufahamu hali ya soko.

ATCL yaomba radhi usumbufu safari za anga
TFF yapongeza juhudi za KTO