Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Afrika Mashariki, limeteua Watanzania wanne (4), kuendesha michuano ya kuwania Kombe la Chalenji inayoandaliwa na CECAFA.

Watanzania hao ni Alhaji Ahmed Mgoyi aliyeteuliwa katika Idara ya Mashindano huko CECAFA wakati mwingine ni Sunday Kayuni ambaye ameteuliwa katika Idara ya Ufundi.

Mgoyi ameteuliwa kutokana na uzoefu na uwezo wa  wake wa kusimamia mashindano ya kimataifa huku akiwa na rekodi ya kusimamia vema mashindano hayo yalipofanyika kwa mara ya mwisho nchini Tanzania mwaka 2015 wakati Kayuni ni Mkufunzi anayetambuliwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Wengine ambao wameteuliwa kuendesha michuano hiyo ni Waamuzi wawili.

Waamuzi  hao ni Elly Sasii (mwamuzi wa kati) na Soud Lilla (Mwamuzi Msaidizi). Tayari wateuliwa wote wako Kenya kwa ajili ya michuano hiyo.

Mwamuzi mtanzania kuchezesha kombe la dunia 2018
Ratiba ligi Tanzania bara, kombe la Azam