Watanzania Kennedy Chatengwa (52) na Chrispine Nicholaus (50) wameuawa vibaya kisha miili yao kukatwa na kuchomwa moto kutokana na tuhuma za kuwa wachawi nchini Zambia.

Mbali na vifo hivyo vilivyotokea katika kijiji kilichopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mwanamke mmoja ambaye aliongozana na Marehemu naye amejeruhiwa vibaya na amelazwa Hospitali akiendelea na matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa, Justine Masonje amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema waliofariki dunia walikuwa wakazi wa Kata ya Manbwekenya iliyopo Wilayani Kalambo mkoani humo.

RPC Masonje ameongeza kuwa Watanzania hao ni miongoni mwa watu 50 walioripotiwa kuuawa nchini Zambia kutokana na imani za kishirikina.

Sura bajeti ya 2020/21, Uchaguzi mkuu wapewa kipaombele
Video: Nguvu ya umma, Mashinji, Mdee, Bulaya, Matiko 'OUT' Mbowe bado