Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand inayofahamika kama Tanzanians in Thailand (TIT), imepata viongozi wapya kupitia mkutano mkuu uliofanyika Novemba 7 mwaka huu jijini Bangkok.

Jumuiya hiyo inahusisha watanzania mbalimbali wakiwemo wanafunzi, wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya kazi nchini Thailand kwa lengo la kusaidiana katika mambo mbalimbali muhimu.

Mkutano huo mkuu wa TIT ulifanya uchaguzi na kumchagua Bw. Maumba Mgaya kuwa mwenyekiti na Bw. Alois Ngonyani kuwa Mwenyekiti msaidizi huku nafasi ya Ukatibu ikienda kwa Bw. Andrew Wajama na msaidizi wake ni Bw. Emmanuel Mushi.

 

Wanachama wa TIT wakipata Chakula baada ya Kufanya Uchaguzi

Wanachama wa TIT wakipata Chakula baada ya Kufanya Uchaguzi

Wengine waliochaguliwa ni Emmanuel Nyamageni (Afisa Mawasiliano), Jordan Hosea (Afisa Mawasiliano Msaidizi), Adolf Kigombola (Mhazini), Tumaini Kalindile (Mhazini Msaidizi).

Kupitia tukio hilo lililoambatana na tafrija fupi chini ya udhamini wa kampuni ya Broadhurst Pacific, uongozi huo mpya uliwashukuru viongozi waliomaliza muda wake mpya kwa kazi waliyoifanya na kufanikisha uchaguzi huo.

“Tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.”

Jumuiya hiyo pia ilitoa wito kwa watanzania wote waishio nchini Thailand na wanaotarajia kuingia nchini humo kuwasiliana na Jumuiya hiyo kupitia namba ya simu +66947230002/ +66972494819 na kushirikiana nao kwani umoja ni nguvu.

Tukio hilo la uchaguzi liliambatana na sherehe fupi ya kumpongeza Bi. Magreth Dionis Mjindo kwa kumaliza Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii ambapo anatarajia kurudi nyumbani Tanzania kulitumikia Taifa.

Ndugu Florean akimkabidhi Bi. Magreth kwa niaba ya TIT

Ndugu Florean akimkabidhi Bi. Magreth kwa niaba ya TIT

 

 

Islamic State latangaza kuhusika na shambulizi la Kigaidi Ufaransa
Magufuli Kiboko, Afuta Kitengo Cha ‘Msosi’ Wa Rais Ikulu