Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni walionao kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijengea uzalendo wa kupenda nchi yao.

Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja – Zanzibar.

Amesema kuwa Tamasha hilo linatarajiwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.

“Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana, kuanzia kwa Wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa muziki, Mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” amesema Mahmoud.

Aidha, amesema kuwa tamasha hilo si la watumbuizaji pekee ambao huhudhuria bali kuna baadhi ya watu ambao huenda kwa ajili ya kujifunza kutoka kwa wengine wanaofanya maonyesho na kufahamiana na wadau mbalimbali.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa makadirio ya haraka, tamasha hilo huchangia kiasi cha Dola za Marekani 7 milioni katika uchumi kila mwaka.

 

 

Makonda atangaza neema waliodhurumiwa mali, atoa siku 5
Video: Mafuriko yazisomba kaya 2,700 Kilosa, Pingamizi na vituko Kinondoni, Siha