Askofu Kiongozi wa Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo, amewaasa Watanzania kuacha kulalamika na badala yuake wajikite katika kufanya kazi njema inayompendeza Mungu.

Askofu Cheyo ametoa kauli hiyo katika ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini.

Amesema kuwa ili Watanzania waweze kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana na mambo ya kisiasa ili waweze kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.

Hata hivyo, ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wake wengine wa dini nchini kutofautisha dini na siasa ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha amani ya nchi.

 

Miguna asafirishwa kwenda Canada
Erdogan, Netanyahu wazidi kushambuliana kuhusu Gaza