Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuwa wazalendo kwa Taifa ikiwemo kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Majaliwa ametoa kauli hiyo Agosti 05, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika ziara yake ya kikazi Wilayani Ikungi mkoani Singida.

Amesema, “Nawapongeza Madiwani kwa mpango wenu wa kupanga mji huu na ninataka niwambie wananchi msikwamishe maendeleo, lazima kila mmoja awe na uzalendo kwa Taifa hili.”

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa Halmashauri ya wilaya hiyo imeweka mpango wa kuendeleza mji wake, na kwamba wananchi ambao maeneo yao yatachukuliwa kupisha mradi huo watafidiwa kulingana na taratibu za uthamini.

Amesema, Mthamini wa Serikali ndiye mwenye dhamana ya vigezo vya fidia, hivyo kuwasihi wananchi hao kutoa ushirikiano wa jambo hilo pindi watakapofikiwa na wahusika.

Basi lagonga na kuwaka moto, wanne wateketea
Rais aridhia kutolewa fedha miradi ya Wananchi