Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City wamejipanga kufanya usajili wa wachezaji watatu ama wanne kwa ajili ya kuboresha kikosi chao kwa msimu wa 2016-17, ambao utaanza rasmi mwezi wa nane (August).

Makamu mwenyekiti wa Leicester City, Aiyawatt Srivaddhanaprabha amesema watafanya usajili wa wachezaji hao wachache, alipofanya mkutano na waandishi wa habari mjini Bangkok ambapo kikosi cha mabingwa hao wa England kilifanya ziara.

Makamu mwenyekiti wa Leicester City, Aiyawatt Srivaddhanaprabha

“Tunajipanga kwa mengi lakini kubwa ni kufanya usajili wa wachezaji wachache, na huenda tukawasajili watatu ama wanne hivi, ambao wataidhinishwa na meneja.”

“Tutazingatia vigezo kadhaa, lakini kubwa tutakalo liangalia ni ushap na uwajibikaji wa mchezaji atakapokua uwanjani, kwani bado lengo letu ni kuendelea kupamabana na kutetea ubingwa wetu msimu ujao.” Alisema Srivaddhanaprabh.

Leicester City, wataanza msimu wa 2016-17, kwa kucheza mchezo wa kuwania ngao ya jamii dhdii ya mshindi wa mchezo wa kombe la FA ( Man Utd Vs Crystal Palace) ambao umepangwa kucheza mwishoni mwa juma hili jijini London.

Hivi Punde: Ndege yapotea angani ikiwa na abiria 66
Randy Lerner Akubali Kunawa, Aipiga Bei Aston Villa