Chelsea itawakosa nyota wake David Luiz, Tiemoue Bakayoko na Ross Barkley katika mchezo wa kesho wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

Luiz anaandamwa na majeruhi ambapo amecheza mechi nne katika michezo 13 ya Chelsea mwaka huu wakati Bakayoko akiwa nae akiumia mapema mwezi huu.

Barkley alicheza mara ya mwisho mwezi iliyopita katika mchezo dhidi ya Arsenal uliomalizika kwa kipigo cha mabao 2-1.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema wachezaji hao wote hawatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya United, “Hapana hawatacheza, lakini hakuna mchezaji mwingine atakaye kosekana baada ya hao wote wako vizuri.”

Chelsea imepoteza michezo miwili mfululizo ya ligi mwezi uliopita ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo huku ikiizidi pointi moja Tottenham Hotspur iliyo nafasi ya tano.

Mwingine abainika kutumia dawa haramu michezoni
Video: Wananchi wafunguka kuhusu hali ya kisiasa nchini