Ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma nchini Misri, inawashikilia wanaume watatu waliokamatwa baada ya kusambaa kwa video inayowaonesha wakiimba na kucheza katika msikiti wa El-Marg, uliopo eneo la kaskazini mashariki mwa jiji la Cairo.

Video hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, inamuonyesha mwanamume akicheza, kuruka na kuimba kwa kipaza sauti cha msikitini kwa muziki wa mwimbaji Ahmed Moza alieimba wimbo wa Mahraganate.

Mahraganate, neno linalojulikana kama sherehe kwa Kiarabu au “electro-chaâbi” imekuwa ni mtindo wa muziki unaosikilizwa zaidi nchini Misri ambao umepata umaarufu zaidi kutokana na mashairi yake.

“Wanamuziki hawa hutumia programu isiyolipishwa inayodaiwa kuwa ni ya bei nafuu kuchanganya muziki wa kitamaduni na sauti za kielektroniki huku wakipata hamasa ya midundo na ghani za kisanii,” alisema mmoja wa watoa maoni Seif Abi.

Kukamatwa kwa watu hao, kunatokana na aina iyo ya muziki kuchukuliwa kinyume na maadili, ingawa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mwendesha mashtaka haielezi kosa halisi la wanaume hao watatu waliowekwa rumande huku wakifanyiwa uchunguzi.

Mona Seif, dadake mfungwa mashuhuri wa kisiasa wa Misri Alaa Abdel Fattah, alisema kwenye chapisho lake la mtandao mmoja wa kijamii kuwa watu hao watatu wamehojiwa na watu wa Usalama wa Taifa.

Hata hivyo inadaiwa tangu aingie madarakani mwaka wa 2013, Rais Abdel Fattah al-Sissi amekuwa akishutumiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa kuwanyamazisha watu, kwa makosa tofauti ya kesi za kigaidi na taarifa za uwongo.

“Sekta huru za muziki na filamu pia zimekuwa zikilalamika mara kwa mara kuwa ziko chini ya shinikizo na haziwezi kupata wafadhili toka nchi ambayo serikali au matawi mbalimbali ya vyombo vya usalama vinashikilia kampuni nyingi zaidi za utayarishaji,” alifafanua Hafidh Dosi.

Mapema mwezi Mei 2022, watu watatu wa sanaa ya uchekeshaji waliachiliwa baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, wakidaiwa kutoa habari za uwongo na ugaidi baada ya kuchapisha wimbo kwenye mtandao wa TikTok wakilaani mfumuko wa bei.

Rais amuondolea madaraka yote Makamu wake
Treni ya abiria yapata ajali Tabora