Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewakamata watuhumiwa watatu wanaohusishwa na kuchoma moto ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Agosti 14,2020 mwaka huu.

Watuhumiwa walikamatwa kwa nyakati tofauti wakati wa uchunguzi akiwemo dereva wa CHADEMA mkazi wa tabata Jijini Dare es Salaam Leonard S/O Cathbert Ntukula, na Prosper S/O Masatu Makonya, Afisa muhamasishaji wa CHADEMA makao makuu na mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Amesema jalada la kesi limepelekwa ofisi ya taifa la mashtaka kwaajili ya kusomwa na kutolewa maamuzi au maelezo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuandaa hati ya mashtaka.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili baada ya kukamilika taratibu za kisheria.

Tetesi za usajili: Koeman kumn'goa Wijnaldum Liverpool, Messi aitetemesha Barcelona
Babu Zlatko Krmpotic aomba muda Young Africans