Bukoba mkoani Kagera Mahakama ya hakimu mkazi  imewahukumu watuhumiwa watatu kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukabiliwa na tuhuma za kula njama na kujihusisha na tukio la uchomaji wa makanisa na kuwakata watu makoromeo.

Ambapo hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bukoba Charles Uiso, amewatolea hukumu hiyo na amesema mahakama imetoa  adhabu hiyo kali kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo wakati kesi ilipokuwa inaendeshwa chini ya sheria.

Hakimu Charles Uisso amesema watatu hao waliotiwa hatiani watatumikia kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kula njama ya kuchoma kanisa adhabu ambayo itaenda sambamba na hukumu ya kifungo cha maisha.

Matukio ya namna hii yanaongezeka kwa kasi sana, utu wa watu umepotea watanzania, miaka hii mtu kumuua mwenzake ni jambo la kawaida sana watu wanakosa hofu ya Mungu.

Serikali kwa kusaidiana na wananchi wafanye uchunguzi wa kina kwa matukio kama haya amabayo sio ya kawaida na hatua kali zichukuliwe.

Sudan yatakiwa kuheshimu mkataba wa Amani
Video: Babu Seya, Papii Kocha waula tena, Clouds washtukia jambo sakata la Masoud Kipanya