Kamati ya uchaguzi ya Klabu ya Stand United ilikutana jana katika Hoteli ya Karena mjini Shinyanga kufanya usaili wa wagombea ambapo wagombea watatu wamepigwa panga.

Jumla ya wagombea 15 walijitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Juni 26 mjini Shinyanga.

Katika usaili huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Paul Kaunda aliwataja walioondolewa kuwa ni Albert Silwimbi, Ally Maganga ma Charles Shigino ambao wote walikuwa wakigombea nafsi ya Ujumbe.

Wagombea waliobakia katika kichang’anyiro hicho ni Emmanuel Kaombwe, Dr Elson Maejaj, Salum Kitumbo na Ibrahim Mbogo wanaogombea uenyeki wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti aliyepenya kwenye mchujo ni mgombea mmoja pekee aliyejitokeza, Luhende Richard.

Kwasasa wajumbe waliosalia ni saba tu ambao kati ya hao, watano pekee ndio watakaochaguliwa na wanachama wao kwa kupigiwa kura. Wajumbe hao ni Miriam Rukandizya, Jackline Isaro, Godfrey Tibakyenda, Fransisko Magoti, Steven Mihambo, Jimrod Mayanga na Twahil Njoki.

Mcameroon Kumsabidili Romelo Lulaku
Sentensi 3 za Waziri Nape kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge