Watu watatu mkoani Tabora wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji  ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahona Pondamali (50)  mkazi wa Wilaya ya Sikonge yanayosadikiwa kutokea Aprili mwaka huu.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mnamo tarehe 22 mwezi wa nne mwaka huu mke wa marehemu aliripoti Polisi kupotea kwa mme wake katika mazingira ya kutatanisha na ndipo Jeshi la Polisi lilipoamua kuanza uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kubaini kuwa mtu huyo akupotea bali aliuwawa.
 
Mtafungwa amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio marehemu alipokuwa akinywa pombe alikuwa na tabia ya kumpiga mke wake na watoto na ndipo walipoandaa mpango wa kumkodi mtu wa kumpiga kwa ajili ya kumrekebisha tabia hali iliyosababisha mauti yake.     
Ameongeza kuwa Polisi kwa kushirikiana na wananchi ndipo walipo gundua kuwa marehemu yuko katika shimo la wachana mbao na kuamua kulifukua ndipo ndugu wa marehemu waliposema kuwa ni ndugu yao aliyedaiwa kupotea
 
Hata hivyo, Mtafungwa amewataja wanaotuhumiwa kwa mauaji hayo na wanaoshikiliwa na Polisi kwa uchunguzi kwa tuhuma za mauaji kuwa Mke wa Marehemu, Tatu Said (30) , mtoto wa marehemu Katambi Mahona (13) na jamaa wa kukodi Mwanza Mburuka(31).
 

Manispaa ya Ilala yapewa onyo kali, yatozwa milioni 25 kwa uchafuzi wa mazingira
Serikali yapunguza gharama za dawa, vifaa tiba na huduma za afya