Katika kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar wapo Mkoani Tanga ambapo pia watafanya mkutano wa mwaka wa Dawati hilo pamoja na kufanya zoezi la kutoa elimu ya kuepukana na vitendo vya Ukatili katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Afisa wa Jeshi la Polisi akiendelea na zoezi la utoaji wa Elimu

Wakati wa zoezi hilo, maeneo yaliyofikiwa ni pamoja na Shule za Msingi na Sekondari, Vijiwe, Masoko na kwenye mikusanyiko yenye watu wengi ambapo kwa pamoja Watendaji hao wametoa elimu kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali za Mitaa na Kata pamoja na Maafisa Ustawi Jamii.

Mtendaji wa Dawati la Jinsia akiwa amejumuika na Watoto wakati wa zoezi la utoaji Elimu.

Utaratibu huo wa kutoa Elimu, umelenga kuzifikia pia baadhi ya Wilaya za mkoa huo hususani katika maeneo ya Barabara kuu ambayo yana mikusanyiko mikubwa ya watu, ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Wadau wa Habari wataka ushirikishwaji utungaji wa Sheria
Serikali yazidisha vita ujangili wanyamapori, mazao ya misitu