Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Ally juma ameagiza watendaji wa kata zilizoshinda katika kampeni ya afya na usafi wa mazingira kufika ofisini na kuchukua pikipiki zao huku usajili wa piki piki hizo ukifuata.

Mkurugenzi ametoa uamuzi huo katika kikao cha kubadilishana uzoefu na kujiwekea malengo ya kufikia asilimia 100 katika kampeni hiyo mwaka wa fedha wa 2019-2020 mara baada ya piki piki hizo kukaa muda mrefu bomani zikisubiri usajili.

Video: Wakili Manyama atoa ufafanuzi kuhusu sheria ya kodi

“serikali ilitupatia zawadi ya gari mbili na piki piki 14 baada ya kushinda katika kampeni ya afya na usafi wa mazingira na gari zile zinatusaidia sana katika utekelezaji wa kampeni hii, lakini bado kuna piki piki hazijatoka bomani sasa nimeshaelekeza kwasababu zinasubiri usajili basi ziende kule kule kwenye kata husika zikifanye kazi kwasababu zinafanya kazi maalumu kwa hiyo kesho zitatoka zote na kila mtendaji hapa akachukue piki piki yake”alisema Juma

Mkurugenzi huyo amesema kufika tarehe 15 usajili wa piki piki hizo utakuwa tayari hivyo kuwapelekea watendaji katika maeneo yao kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiskia zawadi walizopewa bila kuziona.

BAJETI: Serikali kuongeza kodi ya nywele bandia hadi 25%, kuongeza mapato

Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekuwa ikitekeleza kampeni ya usafi wa mazingira katika ngazi ya mkoa na kitaifa na kupelekea kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika utekelezaji wa kampeni hiyo kwa miaka 6 mfululizo tangu mwaka 2013-2018 ilipoanza kampeni hiyo kwa kupata asilimia 99.

2018-2019: Pato la Mtanzania laongezeka kwa Sh 100,000

LIVE IKULU: Rais Magufuli katika hafla ya jioni na Rais wa DRC Felix Tshisekedi

Video: Bajeti funga kazi, kigogo CHADEMA auawa nyumbani kwake usiku
Video: Mzee Kilomoni hana chake Simba, anapoteza muda-Magori