Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kuhakikisha suala la taarifa chafu za Watumishi linamalizika haraka iwezekanavyo ili kurahisisha zoezi la uhakiki wa taarifa za kiutumishi kwenye Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Susan Mlawi alipokuwa katika kikao kazi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na  Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

“Sitegemei tena kusikia Halmashauri au Mkoa una taarifa chafu za watumishi wake, hivyo nawaagiza Maafisa Utumishi na Watendaji katika Mikoa na Halmashauri mhakikishe suala hili linafikia ukingoni,” Amesema Susan.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu ,Ofisi ya Rais-Utumishi, Leornad Mchau amesema kuwa taarifa chafu za watumishi ni eneo ambalo linasababishwa na uwepo wa watumishi hewa.

 

Video: Makonda awageuzia ubao maafisa elimu Dar
Mbunge wa Kibaha awakumbuka wananchi wake