Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdulla Said amewasihi Watendaji wa idara na vitengo vya Wizara hiyo kujitathimini kiutendaji na badala yake watekeleze wajibu wao na kuongeza ubunifu kiutendaji.

Nasaha hizo zimetolewa wakati akizungumza na watendaji wa idara ya Elimu ya Mbadala na Watu Wazima pamoja na Bodi ya Mikopo Zanzibar, huko katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo Mazizini Zanzibar.

Amesema, Wizara hiyo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya nchini kwani ina dhamana ya kusimamia uzalishaji na upatikanaji wa wataalamu wenye uwezo na waliobobea katika fani mbalimbali nchini.

Aidha Said ameongeza kuwa ni lazima watendaji hao wawe mfano wa kuingwa katika masuala ya utendaji,nidhamu,kujituma na ubunifu katika sehemu zao za kazi ili kwenda sambamba na kasi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Hussein Ali Mwinyi kiutendaji.

Walimu wekeni ukaribu na wenye ulemavu - TAMWA
Idadi ya wajane inaongezeka kwa kasi - Rais Dkt. Mwinyi