Watalii 150 kati ya 800 wanaotarajia kuingia nchini kutoka Israel kwaajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii wamewasili jana.

Akizungumza baada ya kuwapokea watalii hao katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), Mwenyekiti wa bodi ya utalii Tanzania (TTB), Jaji msaafu Thomas Mihayo amesema hadi kufika Desemba 31 watalii 800 watakuwa wamewasili nchini na watakaa kwa siku nne.

“Hawa watalii waliowasili watakuwa hapa nchini kwa siku nne, watatembelea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, hifadhi za taifa Manyara, Tarangire, Serengeti na Bonde ya eyasi ambako watajifunza tamaduni za wananchi wanaoishi eneo hilo” amesmea Jaji Mihayo.

Ameongeza kuwa katika kipindi kifupi Tanzania italiteka soko la utalii barani Asia baada ya watalii wanaotutembelea kuendelea kuwa mabalozi wazuri wanaporejea nchini mwao.

Mkurugenzi mtendaji wa TTB, Devotha Mdachi amesema watalii wanaokuja nchini wanavutiwa na tamaduni mbalimbali zilizopo nchini pamoja na weledi walionao waongoza watalii wetu.

Miongoni mwa watalii waliofika kwa mara ya kwanza kutembelea Afrika aliyetoka Israel, Omrif Shlom amesema amefurahishwa na ukarimu walioonyeshwa baada ya kuwasili uwanja wa Kia jana.

Hata hivyo Desemba 24 na 25 watalii kutoka Israel watakuja nchini kukamilisha idadi ya watalii 800 ambao wamethibitisha kutembelea vivutio vya utalii.

 

Maiti yagoma kuzikwa kisa kulipiwa mahari
Daktari mbaroni kwa wizi wa dawa, vifaa