Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia  watoto 113 kati ya umri miaka 8 hadi 15 kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu ikiwemo matukio ya uwizi, uvunjaji, ukataji wa mapanga katika Wilaya ya Nzega na Manispaa ya Tabora katika kipindi cha kuanzia Agosti na Septemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Polisi mkoani Tabora ACP Safia Jongo amesema kuwa kukamatwa kwa watoto hao kunafuatia msako unaoendelea mkoani hapo kukamata wahalifu mbalimbali kwa kipindi cha mwezi moja .

Aidha watoto wanatumia majina kwa ajili ya vikundi vyao wa Tabora manispaa wanatumia jina la Nunda na wa Wilaya ya Nzega walitumia majina ya Roho saba na Roho mbili.

Kamanda Sofia amesema watoto hao wanafanya uhalifu kwa kuwapora hadi kuwajeruhi watu kwa kushirikiana na watu wazima ambao wamekuwa wakiwatuma kufanya uhalifu huo na wengine wanavamia majumbani.

Katika Manispaa ya Tabora wamekamatwa watoto 96 na Nzega watoto 17 jambo ambalo ni hatari sana kwa wazazi kushindwa kuwalea watoto wao .

Hata hivyo baadhi ya watoto wamefikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Wezi vifaa vya magari mjipange: RC Makalla
Neema yawashukia bodaboda