Kituo cha Association For Termination of Female Genital Multilation (ATFGM ) kilichopo Mkoani Mara kimesema jumla ya watoto 67 wamekataliwa na familia zao baada ya kukataa kukeketwa na kukimbilia katika kituo hiko.

Kituo hicho cha (ATFGM), ambacho kazi yake ni kuhifadhi wasichana wanaokataa kutekeleza mila hiyo.

Akifungua mafunzo ya madhara ya ukeketaji na tohara katika kituo hicho cha (ATFGM), Kaimu ofisa elimu msingi wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Amos Waitara amevitaka vyombo husika vya Serikali kuhakikisha watoto hao wanapata haki za malezi kutoka kwa wazazi wao.

“Hatuwezi kulifumbia macho suala hili kwa baadhi ya wazazi hawa kuminya uhuru wa watoto ,walioona mbali na kuchukua jukumu la kupinga vitendo vya kikatili vya ukeketaji, wazazi hao waitwe na kueleza kwa maandishi sababu za kuwanyanyasa.,”amesema Amos Waitara.

Aidha Meneja miradi wa ATFGM  , Valerian Mgani amesema tangu kituo hicho kilipoanzishwa mwaka 2008 wamekuwa wakipokea watoto ambao wanakimbia ukeketaji kutoka Wilaya za Tarime,Serengeti na Loliondo Mkoani Arusha.
 

Video: TRA yabadili utaratibu wa ulipaji kodi
Familia ya Nguza Viking "Babu Seya" yatinga Ikulu