Jeshi la polisi mkoani Rukwa limewarejesha nyumbani kwao watoto nane waliofichwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni viongozi wa dini ili kuwaunganisha na wazazi wao katika kijiji cha Namansi, kata ya Ninde kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, waweze pia kuendelea na masomo yao.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi, George Kyando ambaye aliongoza viongozi mbalimbali wa mkoa wa Rukwa ikiwa ni pamoja na Afisa uhamiaji, Afisa magereza, afisa ustawi wa jamii na wengineo, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namansi na vitongoji vyake, amewataka waache mara moja tabia iliyojengeka miongoni mwao ya kuwaamini hata watu wasiowajua,na kuwakabidhi watoto wao kwa tamaa ya fedha jambo ambalo ni la hatari mno.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kijiji hicho pamoja na wa kata ya Ninde,akiwemo diwani wa viti maalumu, Janeth Kashamakula, wameikemea mno tabia inayoanza kuota mizizi hasa kwenye kitongoji cha Chele, ya kuwapokea wageni kwenye maeneo yao na kuingia nao makubaliano mbalimbali bila hata ya kuushirikisha uongozi wowote.

Kidudu mtu chaibua taharuki Mwanza
Matukio miaka 15 ya Saida Karoli (Picha 33)