Shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) limesema kuwa duniani kote watoto zaidi ya milioni 100 wa kike na kiume wanatumikishwa kazi ngumu ambapo asilimia 70 wanafanya kazi katika sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji wa samaki na misitu.

Kwa mujibu wa FAO idadi hiyo imeongezeka  kutoka watoto milioni 10 tangu mwaka 2012, licha ya jitihada za Umoja wa Mataifa za kutokomeza utumikishaji watoto kwenye sekta hizo.

Hata hivyo ripoti imeeleza kuwa sababu kubwa ni umasikini kwenye familia ambapo wazazi hutumia watoto wao kufanya kazi kwenye kilimo na baadae kudumaza ustawi wa kimaendeleo hasa katika elimu.

Aidha watoto wamekuwa wakikumbwa na madhara ya kiafya kutokana na kemikali zinazotumika kwenye sekta ya kilimo na mara nyingi wazazi hutumia watoto wao kwa kuwa wanafanya kazi bila ujira

Ariane Genthon ambaye anahusiska na programu ya FAO ya kuondokana na utumikishwaji wa watoto kwenye kilimo amesema watoto wanapotumikishwa kwenye kilimo wanashindwa kwenda shule, na hata pale wanapokwenda wanakuwa wamechoka na wanashindwa kusoma ipasavyo kama wenzao ambao hawaendi kwenye kilimo.

 

Marekani yaijibu Iran, 'Chagua moja kusuka au kunyoa?'
DataVision yafanikisha kupatikana mshindi wa tuzo za X-Prize, yashiriki utoaji tuzo Marekani

Comments

comments